Singida Black Stars, Mashujaa FC na Tabora United FC wanasema Simba na Yanga SC au Azam FC ndiyo kina nani Ligi Kuu ya NBC?

NA DIRAMAKINI

LEO Septemba 14,2024 michezo miwili ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara imepigwa katika viwanja viwili tofauti huku matokeo yakiwa ni sare tasa.
Katika dimba la Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora,Tabora United imemenyana na Prisons FC ambapo hadi dakika 90 zinatamatika hakukuwa na mbabe.

Wakati huo huo, sare nyingine ya 0-0 baina ya Azam FC na Pamba Jiji FC imerekodiwa katika dimba la Azam Complex lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Aidha,hii ni sare ya pili mfululizo kwa Azam FC msimu huu na ni mechi ya pili mfululizo kwa Azam FC kwenye Ligi bila kufunga bao lolote.

Mechi ya kwanza ya Azam dhidi ya JKT Tanzania ilimalizika kwa sare tasa ya 0-0.

Katika ligi hiyo yenye timu 16, Singida Black Stars FC wapo kileleni kwa alama zao tisa, Mashujaa FC nafasi ya pili kwa alama saba huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Tabora United kwa alama saba pia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news