Stars ugenini kama nyumbani, thamani ya Squad ya Guinea ni mara 38 ya ile ya Stars

NA MCHAMBUZIHURU

WENGI hawakutarajia kuwa Stars tutashinda leo, lakini binafsi niliamini hata kama hatutashinda, lakini hatutapoteza, kwa nini? Kwa sababu, nimejifunza kitu hamasa nyingi mitandaoni, ni kama huwa inawavuruga wachezaj.
Stars ikijiendeaga kimya kimya lazima ifanye wonders. Ilienda Zambia kimya kimya ikawaduwaza Wazambia, imeenda huko Guinea kimya kimya bila heka heka za mitandaoni, imewaduwaza sio Guinea tu bali hata baadhi ya mashabiki wa soka nchini, hawajaamini.

Kwa thamani ya kikosi cha Stars kinaingia mara 38 kwa kile cha Guinea. Thamani ya Guinea ni Euro 76.83m sawa na Tshs 230.4b wakati Stars thamani ya kikosi ni Euro 2.13m sawa na Tsh 6.3b.

Wakati mchezaji wa thamani kubwa wa Guinea Mlinzi Abdoulaye Toure anayecheza Le Havre AC ya Ufaransa, ana thamani ya Euro 3m sawa na Tsh 9b, wa Stars wa thamani kubwa ni Novatus Miroshi wa Goztepe ya Uturuki mwenye thamani ya Euro 700,000/- sawa na Tsh 2.1b.

Katika FIFA ranking,Guinea ni ya 77, Stars ni ya 113. Kwa hiyo utaona kabisa Guinea wametuzidi kila kitu, ispokuwa kitu kimoja tu, determination ya players wetu.

Asante Stars, mmeonyesha kuwa kumbe mnaweza hata ugenini,tena zaidi ya yumbani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news