Taasisi 40 zajitokeza kutoa elimu ya mpiga kura

DAR-Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi. Angelista Kihaga amesema,tangu kutangazwa kwa nafasi za kutoa elimu ya mpiga kura kwa umma zaiidi ya taasisi 40 zimejitokeza zikihitaji kupewa dhamana hiyo kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba,mwaka huu.
Bi.Kihaga amesema hayo katika mahojiano Mubashara yaliofanyika kupitia kituo cha Televisheni cha TBC kupitia taarifa ya habari.

Amesema,kumekuwa na mwitikio mzuri na mkubwa tangu Waziri mwenye dhamana ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Mohamed Mchengerwa alipotoa tangazo la uchaguzi na kuruhusu matukio mengine kuendelea.

Amesema, zoezi lililopo ni kupokea maombi ya taasisi mbalimbali ambazo zitajihusisha na kutoa elimu ya mpiga kura.

Amesema, baada ya kupokea maombi hayo, zoezi litakalofuata ni kupokea maombi ya taasisi ambazo zitapenda kufanya uangalizi wa ndani wa uchaguzi huu na baadae yatafanyiwa uchambuzi na kupewa kibali kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za Serikali za Mitaa.

Pia, ameongeza kuwa, taasisi yeyote inayohitaji kuomba kutoa elimu ya mpigakura mwisho ni Septemba 6,2024 hivyo waendelee kuomba na zile taasisi zinazotaka kuangalia uchaguzi wa ndani ni lazima ziwe na sifa zote ambazo zimeainishwa katika tangazo.

Ametaja miongoni mwa sifa hizo kuwa ni lazima iwe imesajiliwa na mamlaka inayohusika na usajili huo,na mwisho wa kuomba ni Septemba 17,2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news