TAKUKURU yamtunuku Nathanael Atanas tuzo na shilingi milioni 5

DAR-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imemtunuku Tuzo na fedha taslimu shilingi milioni 5, Nathanael Atanas Mpasi.
Ni kwa kuonesha umahiri kupitia maandiko yanayokemea na kushauri namna ya kudhibiti rushwa katika sekta mbalimbali nchini.

Mpasi amekabidhiwa zawadi hizo Septemba 21,2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa wa taasisi hiyo,Bi.Sabina Seja, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,Crispin Francis Chalamila.

Hafla hiyo ambayo iliandaliwa Johari Rotana Hotel na JamiiForums ilikuwa mahususi kuwatunuku wadau walioshiriki na kuandika ‘Stories of Change’ zitakazoleta mabadiliko katika jamii nchini.Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ni taasisi ya umma inayotekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Moja ya majukumu yake kulingana na sheria hiyo ni pamoja na kushirikisha jamii katika mapambano dhidi ya rushwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news