NA GODFREY NNKO
WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) umerekodi mafanikio makubwa ndani ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 26,2024 na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Ephata Mlavi katika kikao kazi kati ya wakala huo na wahariri wa vyombo vya habari.
Sambamba na waandishi wa vyombo vya habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) jijini Dar es Salaam.
Amesema, katika kipindi hicho wakala huo umekamilisha miradi 38 ambayo inajumuisha kilomita 1,198.5 za barabara,madaraja makubwa tisa na viwanja vya ndege saba, miradi hiyo ni ndani ya mikoa 17.
"Jumla ya kilomita 15,343.88 zimekuwa kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji. Kilometa 1,198.50 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
"Kilometa 2,031.11 ziko kwenye hatua za ujenzi kwa kiwango cha lami. Jumla ya kilometa 2,052.94 na madaraja mawili yamefanyiwa upembuzi yakinifu tayari kujengwa kwa kiwango cha lami."
Miongoni mwa mikoa hiyo ni Simiyu, Arusha, Dar es Salaam, Geita,Pwani, Tabora, Songwe na Ruvuma,Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Iringa, Katavi, Kigoma, Mara, Mbeya na Geita.
Mhandisi Mlavi ametaja viwanja vya ndege ambavyo vimekamilika kuwa ni Julius Nyerere (Terminal Three), Mwanza, Mtwara, Songea, Songwe (runway), Songwe (uwekaji wa taa za kuongozea ndege) na Geita.
Aidha, amesema kuwa miradi nane ya viwanja vya ndege inaendelea ikiwemo Iringa, Msalato, Musoma, Tabora, Shinyanga, Sumbawanga, Kigoma na Moshi.
Amesema, madaraja makubwa ambayo yamekamilika ni lile la Gerezani,Tanzanite jijini Dar es Salaam, Wami mkoani Pwani, Kitengule mkoani Kagera.
Madaraja mengine yaliyokamilika ni Kyegeya, Ruaha mkoani Morogoro,Ruhulu mkoani Ruvuma, Mpwapwa mkoani Dodoma na Msingi mkoani Singida.
Vilevile ameyataja madaraja makubwa ambayo yanaendelea na ujenzi kuwa ni Pangani mkoani Tanga, J.P Magufuli mkoani Mwanza.
Mengine ni Lower Mpiji mkoani Dar es Salaam,Mbambe mkoani Pwani na Simiyu mkoani Mwanza.
Katika hatua nyingine amesema kuwa, madaraja 19 yanatarajiwa kujengwa na Serikali ikiwemo Godegode Mtera mkoani Dodoma na Ugala mkoani Katavi.
Kamshanga, Kyabakoba na Kolebo mkoani Kagera, Bujode, Bulome na Ipyana mkoani Mbeya yanatarajiwa kujengwa.
Mengine ni Chakwale, Nguyami, Mkundi, Mjonga, Dama, Mkondoa mkoani Morogoro, Lower Malagarasi mkoani Kigoma, Songa mkoani Songwe, Kilambo mkoani Mtwara na Chemchem mkoani Singida yapo katika michakato.
Ameeleza kuwa, miongoni mwa barabara ambazo zimekamilika ni Wasso hadi Sale kilomita 48, Kituo cha Forodha Vigwaza, upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge kilomita 12.9.
Nyingine ni Usesule hadi Komanga kilomita 115.2,Komanga hadi Kasinde kilomita 112.8,Kasinde hadi Mpanda kilomita 105.39,Mpanda-Kibo hadi Usimbili kilomita 35, Kidawe hadi Kasulu kilomita 50.
Mhandisi huyo ametaja nyingine kuwa ni Nyakanazi hadi Kibondo kilomita 50,Makutano ya Nduta hadi Kanbigo kilomita 62.50, Makutano hadi Natta kilomita 50 na Chunya hadi Makongorosi kilomita 39.
Nyingine ni Kikusya hadi Ipinda hadi Matema kilomita 34.6, Rudewa hadi Kilosa kilomita 24, Mtwara hadi Mnivata kilomita 50, Maswa Bypass kilomita 11.3.
Mhandisi huyo ametaja barabara nyingine kuwa ni Bulamba hadi Kisorya kilomita 51,Lusitu hadi Mawengi kilomita 50,Sabasaba hadi Sepuka-Ndago hadi Kizaga kilomita 77.4.
Moranga hadi Makete kilomita kilomita 53.5,Sumbawanga-Matai hadi Kasanga kilomita 112, Mpemba hadi Isongole kilomita 50.3, Kazilabwa hadi Chagu kilomita 36, Nyahua hadi Chaya kilomita 85.5 na Maswa hadi Bariadi kilomita 49.7.
Mbali na hayo, amesema wakala huo umepokea fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kusimika taa za barabarani nchini kote.
"Mikoa ambayo tayari imekwisha simikwa taa hizo kwenye baadhi ya barabara zake ni Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Geita, Iriinga, Kagera, Kigoma, Kilimajaro, Lindi, Manyara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida, Songwe, Tabora, Tanga."
Tags
Dr Samia Suluhu Hassan
Habari
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
Kikao Kazi Msajili wa Hazina
Ofisi ya Msajili wa Hazina
TANROADS Tanzania