MAPUTO-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa, Tanzania ilitoa mchango mkubwa katika harakati za kupatikana kwa Uhuru wa Msumbiji, ikizingatiwa kwamba Chama cha Frelimo kilianzishwa Dar es Salaam mnamo mwaka 1962 chini ya uongozi wa Hayati Eduardo Chivambo Mondlane.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika Sherehe za Miaka 50 ya Siku ya Ushindi zilizofanyika katika kiwanja cha Matola, Msumbiji.
Vile vile, Rais Dkt. Mwinyi amesema siku ya maadhimisho hayo yana umuhimu mkubwa kwetu sote kwa kutambua mchango wa Tanzania katika kusaidia kupata uhuru pamoja na kuwa sehemu ya historia hiyo.
Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa, Tanzania na Msumbiji zitaendelea kuimarisha uhusiano wake kwa sababu nchi hizo mbili zinashirikiana katika nyanja nyingi zikiwemo za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kitamaduni, na udugu uliopo.

Pia, ameitakia Msumbiji uchaguzi mwema na wa amani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba,2024.