Tanzania yakaribisha wawekezaji madini mkakati

BALI-Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amesema,Tanzania inakaribisha wawekezaji wote wa madini mkakati na kuweka msisitizo kwamba uongezaji thamani wa madini hayo mkakati lazima ufanyike Tanzania.Mavunde ameyasema hayo leo jijini Bali,Indonesia wakati wa majadiliano juu ya manufaa ya Madini Mkakati katika kukuza uchumi wa nchi wazalishaji ikiwa ni sehemu ya mkutano wa jukwaa la INDONESIA AFRIKA.
Waziri Mavunde ameonesha dhamira njema na mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuvutia uwekezaji nchini na hivyo kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika uchimbaji wa madini mkakati ambayo yana mahitaji makubwa duniani na Tanzania imebarikiwa nayo.
Waziri Mavunde alisisitiza kuwa kwasasa ni sharti la lazima kwamba madini mkakati hayo yaongezwe thamani nchini ili kuvutia viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo betri ya magari ya umeme.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news