Tanzania yatoa uzoefu wake mapambano dhidi ya rushwa Mkutano wa GlobE Network jijini Beijing

BEIJING-Serikali ya Tanzania imeshiriki Kongamano la Tano la Kimataifa la Mashirikiano katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (The 5th Global Operational Network of Anti Corruption Law Enforcement Authorities - GlobE Network) lilofanyika jijini Beijing nchini China.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Francis Chalamila akitoa uzoefu wa Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa.

The 5th GlobE Network Meeting umefanyika Septemba 24 hadi 27, 2024 ukiwa ni mahususi kwa ajili ya Mamlaka za Kuzuia na Kupambana Rushwa Duniani kubadilishana uzoefu na utaalamu katika jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa.

Pia,kongamano hilo, limehudhuriwa na mamlaka 219 za Kuzuia na Kupambana na rushwa kutoka nchi 121 duniani ikiwemo Tanzania ambapo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inashiriki.

Pamoja na mambo mengine, kongamano hilo lilihusisha Warsha ya Wakuu wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana Rushwa kutoa uzoefu wao wa namna Serikali zinavyofanikiwa kudhibiti rushwa katika mataifa yao.

Maeneo yaliyozungumziwa ni pamoja na

1. GLOBAL VISION

2. MFUMO WA KISHERIA NA KITAASISI

3. UENDESHAJI WA GLOBE NETWORK NA

4. KUJENGA USHIRIKIANO

Kupitia warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Francis Chalamila alitoa uzoefu wa namna ambavyo Mfumo wa Sheria na Kitaasisi nchini Tanzania unawezesha mapambano dhidi ya rushwa kufanikiwa.

Mkurugenzi Mkuu alisema, Serikali ya Tanzania imekuwa ikipambana na rushwa kwa kuimarisha mifumo ya sheria na ya kitaasisi ikiwemo kuanzishwa kwa Divisheni ya Mahakama Kuu inayoshughulikia masuala ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Francis Chalamila akifuatilia mada katika mkutano huo.

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu ANTI CORRUPTION AND INSTITUTIONAL LEGAL FRAME WORK IN TANZANIA kwa wakuu wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa wanaoshiriki kongamano hilo.

Aidha, kupitia kongamano hilo, Tanzania ni kati ya nchi 70 zilizopewa fursa ya kutoa wasilisho.

Mtandao wa GlobE ulianzishwa 2021 kwa lengo la kubadilishana taarifa, uzoefu na utaalamu katika mapambano dhidi ya rushwa na TAKUKURU ilijiunga na mtandao huo mwaka 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news