TANZIA:Sista Sesilia Petro Namlamba afariki

RUKWA-Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika (MMMMA) Jimbo Katoliki Sumbawanga, anatangaza kifo cha mpendwa wao Sista Sesilia Petro Namlamba kilichotokea Septemba 25,2024 Kituo cha Afya Katandala alipokua akipatiwa matibabu.
Sista Sesilia Petro Namlamba alizaliwa Mei 25,1923 katika Parokia ya Mkulwe, Jimbo kuu Katoliki la Mbeya.

Maziko yatafanyika Jumatano ya Oktoba 2,2024 katika Makaburi ya Familia Takatifu Kizwite Sumbawanga yakitanguliwa na Adhimisho la Misa Takatifu itakayoanza saa 3:00 asubuhi katika Kanisa la Makao Makuu ya Shirika Katandala, Jimbo Katoliki Sumbawanga.

DIRAMAKINI inatoa pole kwa Uongozi wa Shirika, Ndugu jamaa na waamini wote.
Mpendwa wetu Sista Sesilia apumzike kwa amani, Amina.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news