PWANI-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema mageuzi ya Elimu yanayotekelezwa nchini yanalenga kupata wahitimu mahiri wenye ujuzi ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi.


"Dunia yote hii ni uwanja wa ajira kwa kila mtu, hivyo pamoja na kuwafundisha, tunapaswa kuwapatia ujuzi Vijana wetu ili waweze kujiamini na kutumia fursa mbalimbali za ajira ndani na nje ya Tanzania," amesema Prof. Mkenda.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Mkutano huo Bw. Deo Mbasa amesema Viongozi hao ambao ni Alumni wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wamekutana kutathamini mchango wa Serikali za Wanafunzi katika kuandaa Viongozi wa kesho.
