Tushirikiane kuokoa nguvu kazi ya Taifa dhidi ya dawa za kulevya-Kamishna Jenerali Lyimo

DODOMA-Watanzania wamehimizwa kujitoa kuwekeza kwenye huduma za kuwasaidia waraibu wa dawa za kulevya kwa kuanzisha nyumba za upataji nafuu ili kuokoa nguvu kazi ya taifa iliyopotea kwenye dibwi la matumizi ya dawa haramu za kulevya.
Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, wakati wa mkutano wa wamiliki wa nyumba za upataji nafuu (Sober houses) uliofanyika Dodoma leo, Lyimo amesisitiza umuhimu wa kuongeza idadi ya vituo hivyo ili kukabiliana na tatizo la uraibu wa dawa za kulevya nchini.

"Tunahitaji Sobar houses zaidi, hasa katika maeneo ambayo huduma hii haipatikani kwa urahisi,"amesema Lyimo. 

"Idadi ya wateja wa dawa za kulevya nchini ni kubwa kuliko uwezo wa vituo vilivyopo sasa hivi."
Kamishna Jenerali Lyimo amewataka wamiliki wa nyumba za upataji nafuu (Soberhouses) kuhamasisha wenzao kufungua vituo vipya, akibainisha kuwa kila mtanzania ana nafasi ya kuchangia katika juhudi za kupambana na uraibu wa dawa za kulevya.

"Kufungua Soberhouse sio lazima uwe umewahi kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya. Muhimu ni kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali,"ameongeza.

Kwa upande wao, wamiliki wa nyumba za upataji nafuu wameeleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo, ikiwemo ukosefu wa utambuzi na rasilimali za kutosha. 

Mwenyekiti wa mtandao wa wamiliki wa nyumba za upataji nafuu Hamisi Shuwira, aliomba serikali kutoa vitambulisho vya utambuzi kwa wamiliki wa Sober houses ili kurahisisha kazi yao ya kuwasaidia wateja.

Katibu wa mtandao huo, Saidi Bandawe, amesema, ni muhimu kwa wamiliki wa Sober houses kufuata taratibu zilizowekwa na kutoa taarifa za mara kwa mara.
Ameongeza kuwa,kupambana na uraibu wa dawa za kulevya ni jukumu la kila Mtanzania, si Serikali pekee.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news