DAR-Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.


Ameongeza kuwa, Rais Samia amesimamia maono yake na kuwafanya Watanzania, Afrika na Duniani kote kusimama pamoja naye katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Ameeleza kuwa, Rais Dkt. Samia anathamini watanzania wote bila kujali hali zao na ndio maana ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia inagusa makundi yote ya Wananchi hivyo nao wana wajibu kumuunga mkono katika kuiletea Tanzania maendeleo.