Ubelgiji imeonesha nia kushirikiana na Tanzania nishati safi ya kupikia-Dkt.Biteko

WINDHOEK-Serikali ya Ubelgiji imesema inaunga mkono kampeni ya Nishati Safi ya kupikia na hivyo imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika matumizi ya nishati hiyo kwa maendeleo ya Bara zima la Afrika iliyoasisiwa na Kinara wa Kampeni hiyo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamebainishwa katika Kikao cha Naibu Waziri wa Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko na Waziri wa Nishati wa Ubelgiji, Mhe. Tinne Van Der Straeten kilichofanyika mjini Windhoek, Namibia ikiwa ni sehemu Mkutano wa Nchi za Afika kujadili matumizi Hydrojen kutumika katika kuzalisha umeme.

Dkt. Biteko amesema ili kupata maendeleo ya kweli, Tanzania inatoa kipaumbele katika matumizi ya nishati ambayo itawawezesha kupata maendeleo endelevu ikiwa ni pamoja kuondokana na magojwa na vifo vinavyotokana na matumizi ya nishati isiyokuwa safi.
Amesema ushirikiano wa miaka mingi kati ya Tanzania na Ubelgiji utawezesha upatikanaji wa maendeleo yanayoweza kutokana na uwekezaji wa kimkakati kutoka kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

“Kama mnavyofahamu, Tanzania kupitia Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeasisi na inaendeleza kampeni kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia katika kipindi cha miaka 10 ijayo kuanzia mwaka huu,”amesema Dkt. Biteko na kuongeza kuwa Tanzania ingetamani kuungwa mkono na ubelgiji katika matumizi ya nishati safi ya kupikia kama ambavyo imekuwa ikifafanya katika sekta nyingine ikiwemo elimu na uwezeshaji katika masuala ya usawa wa kijinsia.
Kwa upande wake, Waziri Tinne amesema nchi yake iko tayari kuunga mkono jitihada za matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni mkakati wa kimataifa wa uhifadhi wa mazingira na kuwawezesha wananchi kukuza pato na maendeleo ya kiuchumi.
Amesema matumizi ya vyanzo mbalimbali vya nishati safi ni njia mojawapo ya kuchochea maendeleo ya watu na uchumi wa nchi husika.

Mkutano wa Hydrojen unaoendelea nchini Namibia unalenga kuibua fursa na changamoto zilizopo katika matumizi ya nishati hiyo, ambapo Tanzania itapata fursa ya kujifunza kuhusu matumzi ya Hydrojeni kuzalisha umeme.Mkutano wa Hydrojen unaohudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 5 Septemba, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news