NA DIRAMAKINI
UHAMIAJI FC imepiga Pira Paspoti, Pira Visa ambalo limegeuka adhabu kwa Junguni United kwa matokeo ya mabao 3-1.

Licha ya Junguni United kuanza kwa bao la awali, haikuwa kikwazo kwa Uhamiaji FC kwani Abdulhafidh Salmin dakika ya 46' alisawazisha bao hilo.
Abdulbasit Said dakika ya 65' aliongeza bao la pili kwa Uhamiaji FC huku Daudi Goodluck dakika ya 85' akifunga hesabu.
Katika mchezo wa pili leo Septemba 9,2024 timu ya Mafunzo Sports Club imeibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 ni dhidi ya KMKM.
Bao la Mafunzo limefungwa na Matheo katika
Uwanja wa Annex B (New Amaan Complex) jijini Zanzibar.
Tags
Habari
Junguni United
KMKM
Ligi Kuu ya Zanzibar
Mafunzo Sports Club
Michezo
PBZ Premier League
Uhamiaji FC