DODOMA-Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno, tarehe 18 Septemba, 2024 amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaoendelea katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Ujenzi huo umefikia asilimia 67, unasimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye ni Meneja wa mradi na Mkandarasi ni SUMA JKT.