Ukweli kuhusu madai ya utekaji wa wanachama wa CHADEMA

NA MWANDISHI WETU

KATIKA siku za hivi karibuni, kumekuwa na kauli zinazotia mashaka kwa wananchi juu ya matukio ya kupotea kwa watu nchini.
Watu wengi wamekuwa wakihusisha na kulituhumu Jeshi la Polisi bila kufanya uchunguzi wa kina ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Chama hicho kimekuwa kikitoa madai kuwa, wanachama na wafuasi wake kadhaa wametekwa na Serikali.

Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kwamba madai haya yanakosa ukweli na yanatumika zaidi kama propaganda za kisiasa nchini.

Uhalisia ni kwamba,watu wengi ambao CHADEMA inadai wametekwa na Serikali, kwa hakika ni watu wenye shughuli za kibiashara zinazotia shaka.

Mfano mzuri uliofanyika katika Mkoa wa Rukwa ambao kupitia takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mikoa inayoongoza kwa matukio ya simu za ulaghai hadi kufikia Desemba, mwaka 2023 na idadi ya kwenye mabano ni Rukwa (7,666) na Morogoro (7,171), Dar es Salaam (1,717), Mbeya (1,549), Tabora (590) na Songwe (328).

Kuna uwezekano mkubwa kuwa ndugu Dioniz, ambaye CHADEMA wanadai ametekwa. Uchunguzi unaonesha kuwa, Dioniz alikuwa anajihusisha na biashara zisizo halali, na kutekwa kwake kunahusishwa na biashara zake na wala jeshi la polisi halihusiki.

Ni muhimu kwa umma kuelewa kwamba, Serikali ina jukumu la kuhakikisha usalama wa raia na kushughulikia vitendo vyote vya uhalifu bila kujali itikadi za kisiasa za wahusika.

Madai ya CHADEMA yanaonekana kuwa ni jaribio la kutumia hali hizi ili kuhalalisha ajenda zao za kisiasa na kujionyesha kama wahanga wa mateso ya kisiasa.

Nionavyo, Serikali iendelee kutekeleza wajibu wake wa kulinda sheria na usalama wa nchi bila kubagua, na ichukue hatua stahiki dhidi ya yeyote anayejiingiza katika shughuli za kihalifu, bila kujali ni chama gani cha siasa anachotoka.

Madai ya utekaji wa wanachama wa CHADEMA yanapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa, kwani yanaweza kuwa na nia ya kupotosha umma na kuendeleza ajenda za kisiasa zisizo na msingi.

Mwandishi wa makala haya ni mbobezi wa masuala ya kisiasa, kiuchumi na kiitifaki ana makazi ya kudumu mkoani Ruvuma. Aidha, kilichoandikwa humu ni maoni yake na si ya DIRAMAKINI, unaweza kuyapinga kwa hoja kupitia andiko lako pia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news