VIDEO:Dotto Magari awataka CHADEMA kuwa na moyo wa shukrani kwa Rais Dkt.Samia

DAR-Mshawishi na mhamasishaji maarufu mitandaoni ambaye pia ni muuza magari,Dotto Keto maarufu kama Dotto Magari,mtoto wa Mama Kizimkazi na Hapa Ipo amebisha hodi makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kupitia hodi hiyo kwa CHADEMA, Dotto Magari anawataka viongozi wa chama hicho kuwa na moyo wa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye uongozi wake umefanikisha CHADEMA kupata ofisi yao Mikocheni jijini Dar es Salaam kutoka kupanga Kinondoni.

Dotto ambaye maeneo yake ya kujidai ni huko Kinondoni jijini Dar es Salaam mbali na hayo amepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha nchi inakua na amani.

Vilevile amewataka CHADEMA kuacha siasa za uongo na kumpa Rais Dkt.Samia kongole kwa kazi kubwa anayoifanya.

"Ninyi majirani zetu mlikuwa hamna ofisi kwa takribani miaka 30, leo Mama kajitahidi katoa fungu kawahamishieni ofisi na kupelekwa Mikocheni mnataka nini majirani?."

Dotto Magari amewataka CHADEMA kumuunga mkono Rais Dkt.Samia kwa kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji na ya kufanyia biashara nchini.

“Mnasema nchi haina amani, ni amani gani mnayoitaka? Wawekezaji wamerudi, watu wanafanya wanachotaka,hata nyie mnaongea mnachojisikia, hiyo siyo amani?.

"Mama anafanya kazi kubwa, ameshughulikia umeme, maji, treni ya umeme, barabara kujengwa kwa viwango na viwanda, mpeni Rais Samia maua yake kwani anafanya mengi kwenye hii nchi.

“Mkikaa kwenye vikao vyenu kuweni wakweli kwamba Mama Samia ndiyo kila kitu, apewe mitano yake na akija tena apewe mitano mingine jumla 10, huyu Mama ndiyo aliyeweza kuiongoza hii nchi,”amesisitiza Dotto Magari.
TAZAMA VIDEO CHINI

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news