Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye Viwanja vya Madini Ruangwa kushiriki katika tukio la Hamasa ya Ruangwa Day 2024 leo Septemba 13, 2024. Mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Tanzania, Comrade Mohammed Ali Kawaida.
"Kwa maendeleo haya, mimi na wana Ruangwa hatuwezi tukanyamaza kimya, lazima kumshukuru Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye mimi kwa niaba yenu ninapokwenda kumuambia matatizo yetu kwa niaba yenu hasiti kutupa mabilioni ya fedha, Mama huyu, Dkt.Samia Suluhu Hassan;