Viongozi wa dini Mkalama wahimizwa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa

SINGIDA-Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali amewataka viongozi wa dini wilayani hapa kutumia vyema nafasi zao kuelimisha wananchi kuhusu kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kuhubiri maadili mema nchini.
Wito huo ameutoa leo Septemba 20,2024 wakati wa kikao na viongozi wa dini mbalimbali wilayani hapa kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu mmonyoko wa maadili, suala la uzalendo, amani pamoja na ushiriki wa viongozi hao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

“Ningependa kutumia nafasi hii kuwataka mkawajuze waumini kuhusu kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakofanyika tarehe 27.11.2024 kwa amani na upendo. Tujitokeze kwa wingi katika kampeni, tujiandikishe kwenye daftari la Orodha ya wapiga Kura kuanzia Oktoba 11-20, 2024 lakini pia siku ya uchaguzi tuchague viongizi wetu kwa amani,” amesema Mhe. Machali.

Vile vile, Mhe. Moses Machali amewakumbusha viongozi hao wa dini kuhusu zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutumia nafasi zao kuwaeleza wananchi ifikapo Septemba 25,2024 wajitokeze kuboresha taarifa zao kwa ajili ya uchaguzi mkuu kwa mwaka 2025.

“Uboreshaji utafanyika kwa siku saba kuanzia Septemba 25- Oktoba 1,2024, hivyo tujikoze kwa wingi pia,”amesema Mhe. Machali.

Akizungumzia kuhusu suala la maadili pamoja na amani nchini, Mhe. Moses Machali amesema viongozi wa dini wanajukumu kubwa katika kuhubiri amani pamoja na kulinda maadili ya jamii za kitanzania.

“Twendeni tukahubiri amani na upendo kwa waumini wetu, nitashangaa siku nikisikia watu wa Mkalama wanagombana kwasababu ya dini, kila mmoja aheshimu imani ya mwenzake,” amesema Mhe. Machali.

Kwa upande wake Mchungaji Manase Msengi, kutoka Kanisa la KKT Ushirika wa Nduguti, ambaye amezungumza kwa niaba ya viongozi hao, amemshukuru na kumpongeza Mkuu wa wilaya ya Mkalama kwa kukutana na viongozi wa dini kwa ajili ya kujadili masuala ya maadili, uzalendo na amani hasa katika kipindi hiki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwataka wananchi wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news