Waandishi wasaidizi kata Mkoa wa Singida wapigwa msasa

SINGIDA-Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt.Zakia Mohamed Abubakar ametembelea mafunzo ya Waandishi Wasaidizi ngazi ya Kata watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Singida Vijijini mkoani Singida na kuzungumza nao wakati wa mafunzo yao ya siku mbili yaliyomalizika leo Septemba 19, 2024.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (wapili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia (kulia) wakiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na Maafisa Waandikishaji Wasaidizi Ngazi ya Kata wakati alipotembelea mafunzo yao leo Septemba 19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji Septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi hao Wasaidizi ngazi ya Kata, Dkt Zakia aliwataka kuzingatia mafunzo hayo ili nao waende kuwafundisha wachini yao lakini kubwa ni kuhusu dhamana waliyopewa ya kuendesha zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika maeneo yao.

Dkt Zakia amesema umakini mkubwa unahitajika wakati wa utekelezaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwani daftari hilo ni nyenzo muhimu kwa ajili ya Uchaguzi.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo Septemba 19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba Mosi mwaka huu.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt.Zakia Mohamed Abubakar akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo Septemba 19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu. Katikati ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia na kulia ni Afisa Mwandikishaji Jimbo la Singida Mjini, Bw. Edward Mboya.
Aidha, amewataka kusoma vyema nyaraka walizopatiwa ili kuwa na uelewa mpana utakaowawezesha kutatua changamoto zitakazojitokeza wakati wakutekeleza wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Singida.

"Daftari la wapiga kura ni instrument muhimu sana kwa ajili ya uchaguzi zingatieni mafunzo ili muweze kusimamia uandikishaji wa wananchi na kuboresha vyema taarifa kwa wale wanaoboresha," amesisitiza Dkt Zakia.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joanfaith Kataraia, amemhakikishia mjumbe huyo wa Tume kuwa washiriki wako makini na wana utayari wa kwenda kutekeleza majukumu yao.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia akizungumza.
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Singida Mjini, Bw. Edward Mboya akizungumza.
Washiriki wa mafunzo hayo wakisikiliza nasaha.
Baadhi ya wakufunzi wa mafunzo hayo.

Kataraia amewasisitiza washiriki wa mafunzo kushirikisha wataalamu wa Tume waliopo katika ukumbi wa mafunzo changamoto wanazokutana nazo kulingana na mafunzo waliyopewa kabla ya kumaliza mafunzo ili kuwawezesha kuwa na uelewa wa pamoja.

Mafunzo hayo kwa maafisa waandikishaji ngazi ya Kata yamefanyika kwa siku mbili kuanzia Septemba 18-19, 2024.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt.Zakia Mohamed Abubakar (wapili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia (kulia) wakiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na Maafisa Waandikishaji Wasaidizi Ngazi ya Kata wakati alipotembelea mafunzo yao leo Septemba 19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.
Washiriki wakiendelea na mafunzo kwa vitendo ya matumizi ya mashine za BVR.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar akizungumza na Waandishi wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashautri ya Wilaya ya Singida Vijijini wakati alipotembelea mafunzio yao Septemba 18, 2024. Kushoto ni Afisa Mwandikishaji Francis Mashallo.
Washiriki kutoka kata za Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini wakiwa katika mafunzo hayo.
Washiriki kutoka kata za Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini wakiwa katika mafunzo hayo.

Maafisa waandikishaji wasaidizi Ngazi ya Kata kutoka Kata zote za mkoa wa Singida wamepatiwa mafunzo ya utumiaji wa Mashine za BVR pamoja na ujazaji wa fomu mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Dafrati la Kudumu la Wapiga Kura unaoitaraji kuanza Septemba 25 2024 hadi Oktoba 1 mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news