Wakulima Lindi watakiwa kufuata ushauri wa kitaalam kwenye kilimo

LINDI-Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuachana na maneno ya kusikia kutoka kwa watu wanaowaaminisha kuwa mbolea inaharibu udongo badala yake wafuate ushauri unaotolewa na wataalam wa kilimo ikiwemo kutumia mbolea kwa usahihi kwenye shughuli zao za kilimo.
Ametoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni inayotekelezwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ya Kilimo ni Mbolea.

Uzinduzi uliofanyika katika Kijiji cha Mandawa wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi yenye lengo la kuwaelimisha wakulima kuhusu matumizi sahihi ya mbolea na kuhamasisha usajili wa wakulima kwenye mfumo wa kidijitali wa mbolea za ruzuku.
"Wananchi tubadilike yapo maneno yanasema ukitumia mbolea unaharibu udongo, mbolea ingekuwa inaharibu udongo mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wanaolisha nchi nzima nasisi tukiwepo wasingekuwa wanazalisha mpaka sasa.

"Hayo maneno tunayoyaamini kutoka kwa watu wasiokuwa na utaalam, hawajaenda shule tuachane nayo, tunatumia nguvu kubwa ya kulima eneo kubwa wakati matumizi ya mbolea yangetufanya tulime eneo dogo kwa matokeo makubwa.

"Sisi tunao maafisa kilimo kwenye ngazi ya mkoa,wilaya, kata na vijiji na maafisa hao wana ujuzi unaofanana,hivyo niwaombe wakulima watumieni hao ili wawashauri namna bora ya kulima mazao yanu," Nyundo aliongeza.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa, Farida Kikoleka amesema, huko nyuma suala la kilimo lilikuwa kama adhabu ila kwa sasa wananchi wamebadilika na wanajua kuwa kilimo ni chakula, lakini pia wanajua kilimo ni biashara.

Amesema, kufuatia mwitikio mkubwa wa wananchi waliohudhuria hafla hiyo kuwa mabalozi wa kufikisha ujumbe na elimu ya mbolea waliyoipata kwa wakulima waliokosa fursa hiyo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TFRA, Robert Mtendamema ametoa shukrani kwa uongozi wa mkoa na wilaya kwa kushirikiana kikamilifu katika kuhamasisha matumizi sahihi ya mbolea kupitia kampeni hiyo.
Amesema,Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekusudia Sekta ya Kilimo kukua kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 na kueleza matumizi sahihi ya mbolea yatachangoza kufikiwa kwa lengo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news