Waliotumwa na Afande kumbaka Binti wa Yombo wahukumiwa maisha jela

DODOMA-Leo Septemba 30,2024 Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma (Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki) imewahukumu kifungo cha maisha jela na faini ya shilingi milioni moja kila mmoja washtakiwa wanne wakiwemo Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Magereza.

Ni baada ya kuwakuta na hatia katika makosa yote mawili walioshtakiwa nayo la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile Binti mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.
Kesi hii ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 ilikuwa inawakabili washtakiwa wanne akiwemo MT 140105 Clinton Damas maarufu Nyundo ambaye ni Askari wa JWTZ, Askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson (Machuche) na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Kesi hii maarufu kama Waliotumwa na Afande imesikilizwa faragha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma ambapo upande wa Jamhuri uliwasilisha Mashahidi 18 na vielelezo 12 kuthibitisha mashtaka dhidi ya Washtakiwa.

Washtakiwa walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 19, 2024 na kusomewa mashtaka mawili ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile Binti huyo ambaye mahakamani alitambulika kwa jila la XY.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Zabibu Mpangule washtakiwa hao baada ya kusomewa mashataka walikana na kutokana na unyeti wa kesi hiyo hawakupatiwa dhamana ambapo baada ya kesi kusikilizwa kwa siku kadhaa leo wamesomewa hukumu na kukutwa na hatia hivyo kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news