Wananchi wa Miganga na Nkalakala wahimizwa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa

SINGIDA-Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida,Asia Messos amewataka wakazi wa kata za Nkalakala na Miganga wilayani Mkalama kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Wito huo ameutoa Septemba 4,2024 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata hizo wilayani hapa.

“Mwaka huu tutakuwa na zoezi kubwa la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024, tujitokeze kwa wingi wetu tushiriki uchaguzi huu kwa maendeleo ya kata zetu. Usikubali mtu mwingine akuchagulie kiongozi wakati unauwezo wa kupiga kura,” amesema DED Asia Messos.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi.Asia Messos amesema kuwa ili mwananchi aweze kupiga kura siku ya Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, anapaswa kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo zoezi la uandikishaji litafanyika kuanzia Oktoba 11-20,2024

Aidha, Bi. Asia Messos amewataka wanawake wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi huo kwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili waweze kushiriki katika maamuzi yatayoleta maendeleo ndani ya kata zao.

“Kina mama tujitokeze kwa wingi kuchukua fomu tuwe na viongozi wanawake kwenye nafasi za maamuzi.”
Akizungumzia kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Bi. Asia Messos amesema zoezi hilo kwa mkoa wa Singida linatarajia kufanyika Septemba 25,2024 na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhuisha taarifa zao na ambao hawana kadi wajitokeze kwa wingi kujisajiri ili wapate kadi ya mpiga kura.

Awali akieleza mambo makubwa yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita katika miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bi. Asia Messos amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imepokea zaidi ya Bilioni 60 kwa ajili ya miradi mbalimbali kama vile elimu, afya, michezo, kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news