Wataalamu wa Ununuzi na Mipango waahidi kuchapa kazi kwa vitendo

NA JOSEPHINE MAJURA
WF Mwanza

WAKUU wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango wameahidi kwenda kutekeleza kwa vitendo yote waliyojifunza kupitia mafunzo ya kuwajengea uwezo katika Sheria mpya ya Ununuzi, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi sahihi ya Takwimu yaliyohusisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango iliyohusisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera yakiendelea katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,Sura Na. 103 na Matumizi sahihi ya Takwimu ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Mwanza).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupatiwa mafunzo hayo Afisa Mipango na Uratibu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Bw. Rogatevane Kipigapasi, aliishukuru Serikali kwa kuwajengea uwezo kuhusu Sheria hizo kwa kuwa mafunzo hayo yatawaongezea uwezo na weledi katika kutekeleza majukumu yao.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango iliyohusisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,Sura Na. 103 na Matumizi sahihi ya Takwimu ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

“Kulikuwa na mada nzuri binafsi nimejifunza fursa zilizopo kupitia Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, marekebisho katika Sheria hii yanatoa fursa kwa wazawa kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,”alisema Bw. Kipigapasi.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Kusirie Swai, akizungumza wakati akifungua mkutano wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,Sura NA. 103 na Matumizi sahihi ya Takwimu iliyohusisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mwanza.

Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Bi. Maria Ndohelo, alishauri mafunzo hayo yawe endelevu kwa kutolewa mara kwa mara ili kuhakikisha Sheria, Kanuni na Taratibu zinajulikana vizuri kwa watumiaji wakuu wa Sheria hizo ili iwe rahisi wakati wa utekelezaji.

“Nina waasa Washiriki wenzangu wa mafunzo haya kwenda kuyatumia vizuri tutakaporudi katika Vituo vyetu vya kazi kwa kuwa Serikali ina matarajio makubwa kwetu sisi baada ya mafunzo haya”, alisema Bi. Ndohelo.
Afisa Sheria Mkuu, Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha Bw. Paul Kimweri, akimshukuru Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Kusirie Swai (wakwanza kushoto) aliyekuwa mgeni rasmi baada ya kumaliza hotuba yake wakati wa Mkutano wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango iliyohusisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Bw. Alred Misana, ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mwanza.

Alifafanua kuwa Serikali inawategemea kama wataalamu waliopewa dhamana katika kupanga Mipango ya Serikali na kusimamia Manunuzi mbalimbali ya Umma hivyo ni jukumu la kila mshiriki wa mafunzo kwenda kufanya kazi kwa weledi kama walivyoelekezwa katika mafunzo.
Meneja Huduma za Kanda, Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Juma Mkobya, akichangia mada wakati wa mkutano wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,Sura NA. 103 na Matumizi sahihi ya Takwimu iliyohusisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mwanza.

Mafunzo hayo yamewashirikisha Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango wa mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera yaliyofunguliwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Kusirie Swai katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Kusirie Swai, aliwataka Washiriki wa mafunzo kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.
Mtakwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Philemon Mwenda, akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,Sura NA. 103 na Matumizi sahihi ya Takwimu iliyohusisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mwanza.
Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Bw. Alfred Misana, akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,Sura NA. 103 na Matumizi sahihi ya Takwimu iliyohusisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mwanza.

Bw. Swai alisema kuwa Serikali hutunga sheria ili kuhakikisha wanaotekeleza majukumu kwa niaba ya Serikali wanazifuata, ili kupata matokeo chanya yanayotarajiwa na Serikali.
Meza Kuu ikiongozwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Kusirie Swai (katikati), kutoka kushoto ni Mtakwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Philemon Mwenda, Meneja Huduma za Kanda, Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Juma Mkobya kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Bw. Alfred Misana na Afisa Sheria Mkuu, Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha Bw. Paul Kimweri, wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango iliyohusisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Meza Kuu ikiongozwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Kusirie Swai (katikati), kutoka kushoto ni Mtakwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Philemon Mwenda, Meneja Huduma za Kanda, Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Juma Mkobya kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Bw. Alfred Misana na Afisa Sheria Mkuu, Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha Bw. Paul Kimweri, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango iliyohusisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wanaendelea kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Mipango nchi nzima katika mikoa ya Kikanda ikiwemo Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Pwani, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Magharibi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news