Waziri Balozi Dkt.Chana azindua Zahanati ya Ivilikinge wilayani Makete

NJOMBE-Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amezindua rasmi zahanati ya Ivilikinge iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe sambamba na kukabidhi vifaa mbalimbali vya hospitali vilivyotolewa na Benki ya NMB.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mhe. Chana amesema uwepo wa zahanati hiyo ni miongoni mwa vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan vya kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi mpaka vijijini.

"Hizi ni baadhi ya huduma tulizoahidi kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi hivyo tunapochagua viongozi tuchague ambao watatuletea maendeleo," amesisitiza Mhe. Chana.
Amesema kuwa, kupitia zahanati hiyo wananchi wa Isapulano na vijiji vya jirani watapata huduma bora za afya na kuwaomba wananchi hao kuhakikisha wanaitumia ipasavyo zahanati hiyo.

Naye, Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Willy Mponzi amesema,kwa kuzingatia juhudi za Rais katika kusimamia upatikanaji wa huduma bora za afya mijni na vijijini, changamoto za Sekta ya Afya ni kipaumbele kwa Benki ya NMB kwa sababu afya ni kipaumbele kwa maendeleo ya Taifa lolote.
Kufuatia hatua hiyo,Benki ya NMB inakabidhi vifaa mbalimbali vya hospitali kwa zahanati hiyo ikiwemo Vitanda vya kujifungulia (2),Vitanda vya uchunguzi (2),vitanda vya hospitali (5),Magodoro (5),folding screen (4),folding stretcher (2),delivery kit (5),drip stend(5), mashuka 50 na viti vyenye magurudumu (3) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9.

Awali, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Mganga Mkuu wa Zahanati ya Isapulano, Hassan Omar alisema kuwa mradi huo umegharimu takribani milioni 146.1 ambayo inatokana na michango ya wananchi (milioni 26.5), Wadau wazawa (milioni 6.6, Mbunge wa Jimbo la Makete,Mhe. Festo Sanga (milioni 4) ,Diwani (laki 5 na elfu 30), Benki ya NMB Mabati (milioni 8.5) na Serikali (milioni 100).
Amefafanua kuwa, lengo la mradi huo ni kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Ivilikinge na vijiji vya jirani, kupunguza umbali wa kufuata huduma kwa mama wajawazito, watoto na wazee.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news