Waziri Dkt.Nchemba amuwakilisha Rais Dkt.Samia mikutano ya Taasisi ya Africa50 nchini Madagascar

ANTANANARIVO-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewasili jijini Antananarivo nchini Madagascar, ambapo ameongoza Ujumbe wa Tanzania, akimwakilisha Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM).
Sambamba na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, itakayofanyika tarehe 19 Septemba, 2024, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, na utafunguliwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Andry Rajoelina.
Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Antananarivo, Mhe. Dkt. Nchemba alilakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Madagascar, Mhe. Faustine Kasike na Maafisa waandamizi wa Taasisi ya Africa50, akiwemo Bw. Youssef Abdourabbih, anayehusika na masuala ya Utawala.
Katika msafara huo, Mhe. Dkt. Nchemba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Fedha za Umma (Public Finance Management),Bi. Amina Khamis Shaaban.
Mkutano wa Wanahisa wa Africa50, unatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika na duniani kwa ujumla wakiwemo Wawekezaji kutoka Taasisi za Umma na Sekta Binafsi, wakopeshaji, wataalam wa ujenzi wa miundombinu na kuwawezesha kutafuta suluhisho la changamoto za miundombinu katika Bara la Afrika pamoja na kukabikliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na watahimizana kuhusu matumizi ya nishati safai ili kuchochea uchumi na maendeleo ya nchi hizo.
Africa50 ni Taasisi ya Kifedha yenye Makao Makuu yake Casablanca, Morocco, ambayo imejikita katika nyanja mbili za uwekezaji ambazo ni; Maendeleo ya Miradi na Fedha za Mradi (Project Development and Project Finance) ikiwa na lengo la kuchagiza maendeleo ya miundombinu barani Afrika kwa kuzingatia umuhimu na mchango wa miradi husika kitaifa na kikanda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news