Waziri Dkt.Nchemba ashiriki mjadala kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameshiriki mjadala kuhusu umuhimu wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia, akimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, Mjini Antananarivo, nchini Madagascar.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Africa50, ambaye pia ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, Mjini Antananarivo, nchini Madagascar. Mhe. Dkt. Nchemba, alimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano huo ulioangazia masuala ya ujenzi wa miundombinu inayochochea ukuaji wa uchumi Barani Afrika, pamoja na kupigia chapuo matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuimarisha uchumi wa nchi hizo na watu wake na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na athari za uharibifu wa mazingira.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news