ANTANANARIVO-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ((Mb) ametoa wito kwa nchi za Afrika kutafuta njia na mikakati ya kuboresha uchumi na maisha ya wananchi wake kwa kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni hatua pia ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi yanayochangiwa na uharibifu wa mazingira.
Dkt. Nchemba ametoa wito huo mjini Antananarivo nchini Madagascar kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika leo tarehe 19 Septemba, 2024, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, na kufunguliwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Andry Rajoelina.
Aidha, Dkt. Nchemba alizishauri nchi hizo kuwekeza katika kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa wananchi wao kutumia nishati safi ya kupikia pamoja na faida zinazoambatana na utunzaji wa mazingira kiuchumi na kijamii.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhOVTpeewOPCZRP_TffAP54_j84WAQzFa3tXA3wEFbP2qMCWGfVM9KStMEL2rKu10gA-NfiK5MaF3t3Yt6ofBEQC8TIKcdzo6YO_TFTm3RCQ8jd9rbOeSoTBqwLKB98Rhy9TxN4RWtaucrBTuT7BkF-FUY9KtaQTpbywTNj8CjFEiwTdsTh5XZweh-3y4I/s16000/IMG-20240919-WA0118.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgi8ladID4T7Rffq94oKlVq7lC0SQZuoPSiDu-gqx9TQFuwcB_hLoYK-q0KFEeqTyAKQjqkVpEgGBDtAY2jatLEVfTettVC4Eu53c7R1Iv46DSK821HxlKkhRLiRu7Asbc5NpOlV-JW97CZiSXSlD87DY3SQ4281PkT0mbHMRCiSdqKxZssdoVsIZyLRPo/s16000/IMG-20240919-WA0111.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh1mO4xvXlK8o_jvxFUs73BA3vsxt16xz2HIhNSRp8yTFrLwjc_WYditnMA66fAbK0eYT_BR4oycEErNgqcNzzESN8UNjKUrLWWd9GRYUHprybZVop5j7colw7naHulbEPE-TBYpXm1wylRY7zi1fhdBpXzmrx1tFvXhoZU5GZ33XwrjMYpryaK7DXfWsI/s16000/IMG-20240919-WA0117.jpg)