RUVUMA-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewataka wabunifu wa kazi za sanaa na fasihi kujirasimisha na kurasimisha kazi zao ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa.

"Ili upate fedha za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ni lazima uwe umesajiliwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu Tanzania na ofisi za Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA), pia lazima uwe na TIN namba ya biashara na akaunti namba ya benki kwani mikopo hii kwa sasa inatolewa na Benki ya NBC na CRDB,"amesema Dkt. Ndumbaro.

Washiriki wa mafunzo hayo kwa wakati tofauti wameishukuru Wizara kupitia Mfuko huo kwa kuwapatia mafunzo ambayo yatawasaidia kunufaika na kazi zao ikiwemo kuelewa mikataba wanayoingia na wadau kabla ya kuuza kazi zao pamoja na namna ya kupata faida baada ya kurasimisha.