SINGIDA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika maonesho ya Saba ya Mifumo na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayofanyika mkoani Singida kuanzia tarehe 06 mpaka 14 Septemba, 2024.
Katika maonesho hayo, Benki Kuu ya Tanzania inatoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yake mbalimbali, ikiwemo usimamizi wa mifuko ya udhamini wa mikopo kwa niaba ya Serikali.
Mifuko hii ni pamoja na Mfuko wa Udhamini wa Mikopo ya Mauzo Nje ya Nchi (Export Credit Guarantee Scheme - ECGS) na Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (Small and Medium Enterprises Credit Guarantee Scheme - SME-CGS).Lengo la mifuko hii ni kuwezesha wakopaji wa sekta binafsi na wenye upungufu wadhamana na wanajihusisha na uzalishaji, kupata mitaji kutoka kwenye benki na taasisi za fedha ili kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza uzalishaji, mauzo ya bidhaa nje ya nchi, ajira na mapato ya taifa.