Waziri Lukuvi atoa mitungi ya gesi kwa vijana

IRINGA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani ameendelea kuunga mkono kampeni ya kutumia nishati safi ya kupikia kwa kutoa majiko ya gesi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi ya kata ya mpira wa miguu katika jimbo la Isimani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akigawa majiko kwa vijana wa kijiji cha Kinyika katika Mashindano yaliyohusisha vijiji vilivyo ndani ya kata ya Mlenge.

Waziri ametoa majiko hayo kwa washindi wa nafasi ya kwanza, nafasi ya pili na nafasi ya tatu wakati alipotembelea kata Mlenge mkoani tarehe 29 Septemba,2024 katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo katika vijiji vya Magombwe, Isele, Kinyika na Kisanga vilivyopo katika kata ya Mlenge
“Majiko 1200 yanatarajiwa kutolewa kwa washindi wa mpira wa miguu kwa kata zote za jimbo la Isimani ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Mhe, Rais Dkt, Samia Suluhu Hassani katika kutumia nishati safi ya kupikia,” alisema Waziri Lukuvi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akigawa majiko kwa vijana wa kijiji cha Magombwe katika Mashindano yaliyohusisha vijiji vilivyo ndani ya kata ya Mlenge.

Katika hatua Nyingine Waziri Lukuvi, ameomba wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuendelea kuunga mkono serikali utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa.

Ameongeza kusema utakapofika muda wa uandikishaji kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani, naomba vijana wenye umri wa miaka 18 na kuendelea mjitokeze kujiandikisha uchaguzi wa Mwakani muweze kupiga kura.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani katika matukio tofauti wakati wa Mkutano wa hadhara katika Vijiji vya Magombwe, Isere, Kinyika na Kisanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news