Waziri Mkuu amuwakilisha Rais Dkt.Samia mkutano wa nane wa OACPS

DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 11, 2024 amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) wanaohusika na masuala ya Uvuvi, Bahari, Maziwa na Mito, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Malengo ya mkutano huo ni kuimarisha utekelezaji wa Makubaliano yaliyofikiwa; kuimarisha utekelezaji wa vipaumbele vya kimkakati vya umoja; kubadilishana uzoefu; kuweka mikakati ya pamoja; na kuimarisha ushirikiano na washirika ili kuboresha usimamizi wa bahari, uchumi wa buluu, na maendeleo endelevu ya uvuvi.
Aidha, mkutano huo unatarajiwa kutoa mwongozo wa kimkakati kwenye vikao vya juu vya maamuzi vya Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki ili kuboresha usimamizi wa bahari, uvuvi na ufugaji wa samaki endelevu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news