Waziri Mkuu aungana na Wakuu wa Nchi na Serikali ufunguzi wa UNGA79

NEW YORK-World-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 24, 2024 ameungana na wakuu wa nchi na Serikali katika ufunguzi wa Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79) uliofanyika makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani.
Mkutano huo ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ambapo Waziri Mkuu ameshiriki kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kutoa tamko la Serikali kwenye mkutano huo Septemba 27, 2024 akiwa ni Waziri Mkuu wa Pili kuhutubia baraza la Umoja wa Mataifa. Septemba 27, 2010 aliyekuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda alihutubia baraza la 65 (UNGA65).
Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), pamoja na Balozi wa Tanzania mjini New York, nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Hussein Katanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news