Waziri Ridhiwani Kikwete ateta na wadau wanaoshughulika na masuala ya watu wenye ulemavu nchini

DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amakutana na kuzungumza na wadau wanaoshughulika na masuala ya watu wenye ulemavu jijini Dodoma leo Septemba 2, 2024.
Aidha, katika kikao hicho wamejadili vipaumbele mbalimbali vya kukabili na kutatua changamoto za watu wenye ulemavu ikiwemo suala la mwongozo wa ufikivu wa miundombinu huduma.
Pia,ufikivu wa huduma za afya, uwezeshaji na upatikanaji wa ruzuku,ukamilishaji wa mapitio ya Sera na Sheria ya Watu wenye Ulemavu.

Sambamba na kuwezesha upatikanaji wa unafuu wa gharama za vifaa saidizi ikiwemo suala la kutoa kipaumbele katika majanga, tahadhari na uokozi kwa watu wenye ulemavu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news