Waziri Ridhiwani Kikwete atoa wito kwa vijana wahitimu nchini

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) ametoa wito kwa wahitimu kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kupitia programu ya elimu, mafunzo na uwezeshaji kiuchumi ili kuweza kujiajiri.
Ametoa wito huo Septemba 6,2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Amina Ally Mzee
ambaye alitaka kufahamu mipango ya Serikali kuwezesha vijana kujengewa uwezo ili kuajiriwa au kujiajiri ndani na nje ya nchi.

"Mheshimiwa Naibu Spika ili kuwezesha vijana wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kuwa na uzoefu wa kazi pamoja na sifa nyingine za kujiajiri ndani na nje ya nchi, Serikali inaendelea na programu mbalimbali za mafunzo ya uzoefu wa kazi ikiwemo internship.
"Na maboresho ya Sera ya Taifa ya Vijana ya mwaka 2007 ambayo inahimiza mfumo endelevu wa kuwajengea vijana uwezo na stadi mbalimbali ili waweze kuajirika.

"Kupitia Bunge lako naomba kutoa wito kwa wahitimu kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kupitia programu ya elimu, mafunzo na uwezeshaji kiuchumi kwa kutoa mikopo na mitaji.

"Fursa za ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi katika miradi ya Serikali inayopatikana katika wizara za kisekta na sekta binafsi;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news