Waziri Simbachawene amtembelea Mama Sitti Mwinyi, afikisha salamu za Rais Dkt.Samia

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amemtembelea Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam tarehe 10 Septemba, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024.

“Rais, amenielekeza kuwafikishia salaamu zake na amesema yuko pamoja nanyi na ndio maana amenituma kufika hapa nyumbani na kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi,” amesema Mhe. Simbachawene.

Mhe. Simbachawene amesema Rais Mhe. Dkt. Samia anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene wakifuatilia jambo na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024.

Aidha, Mama Sitti amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake wakati wote bila kuchoka na amemuombea kwa Mungu aendelee kutumia hekima na busara katika kuiongoza Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news