Waziri Simbachawene ateta na Rais mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene tarehe 10 Septemba, 2024 amemtembelea na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiteta na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Simbachawene amefikisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameahidi kuendelea kuwa pamoja na viongozi wakuu wastaafu wa Kitaifa kwa maendeleo ya taifa.

Mhe. Simbachawene amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ina jukumu la kutunza Viongozi Wakuu Wastaafu Kitaifa na Wenza wao, hivyo yuko tayari kuendelea kutekeleza jukumu hilo alilopewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ufanisi.
Hali kadhalika, Mhe. Dkt. Kikwete amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa ujio huo na kupongeza utaratibu uliopo wa kuwatembelea Wiongozi Wakuu Wastaafu wa Kitaifa kwa kuwa unawapa faraja, unaonesha thamani na mchango wao kwa maendeleo ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news