Waziri Soraga azindua Samawa Living Hotel

ZANZIBAR-Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji na wageni ili kuwaondoshea hofu na usumbufu wowote ule unaoweza kujitokeza wanapokuwa nchini.
Samawa Living Hotel inapatikana katika Kijiji cha Paje kilichopo wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja jijini Zanzibar.

Mhe. Soraga amesema hayo Septemba 14,2024 katika hafla ya uzinduzi wa hoteli ya Samawa Living iliyozinduliwa huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema,hoteli hiyo utaongeza idadi ya ajira na kunyanyua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Waziri Soraga ameelezea kuwa, mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazoendelea kufanywa na viongozi wakuu wa nchi, chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Ni katika kuimarisha fursa za uwekezaji na kuvutia uwekezaji mkubwa ikiwemo kuendelea kudumisha amani na utulivu miongoni mwa nyenzo kuu zinazostawisha Sekta ya Utalii nchini.Mhe. Waziri ametoa wito kwa wananchi wa Paje kuendelea kufuata miongozo inayotolewa na Serikali na kuachana na matukio ambayo yataichafua Sekta ya Utalii na nchini.

Naye mmiliki wa Hoteli ya Samawa Living, Riad El Welly ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada kubwa anazoendelea kuzichukua za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news