Waziri wa Fedha aipongeza PPAA kwa kuanzisha Moduli ya kupokea rufaa kieletroniki

ARUSHA-Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.) ameipongeza Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kwa kuanzisha moduli ya kuwasilisha rufaa/malalamiko kwa njia ya kieletroniki.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Bw. James Sando katika banda la PPAA wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha.

Dkt. Mwigulu ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la PPAA katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), na kusema kuwa anaamini moduli hiyo itaisaidia kupata thamani halisi ya fedha.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Bw. James Sando katika banda la PPAA wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha. Wengine Pichani ni Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani, Jaji Mstaafu Mhe. Sauda Mjasiri (kushoto Mwenye Suti Nyeusi), Naibu Katibu Mtendaji wa PPAA, Bi. Florida Mapunda (mwenye suruali ya brauni na koti lenye rangi ya maziwa).

“Napenda kuwapongeza PPAA kwa kuanzisha Moduli hii, nawasihi muendelee kufanya kazi kwa bidii na kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesema Dkt. Mwigulu.

Aidha, Dkt. Mwigulu amefunga rasmi Kongamano la 16 la Ununuzi wa Umma la Afrika Mashariki lililoanza tarehe 9 - 12 Septemba, 2024 jijini Arusha.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Bw. James Sando katika banda la PPAA wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha.

Awali Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Bw. James Sando alisema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu chini ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, PPAA imeweza kushughulikia jumla ya mashauri 140 yaliyotokana na michakato ya Ununuzi wa Umma.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Bw. James Sando katika banda la PPAA wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha. Wengine Pichani ni Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani, Jaji Mstaafu Mhe. Sauda Mjasiri (kushoto Mwenye Suti Nyeusi), Naibu Katibu Mtendaji wa PPAA, Bi. Florida Mapunda (mwenye suruali ya brauni na koti lenye rangi ya maziwa).

“Mhe. Waziri katika mashauri hayo, PPAA ilizuia utoaji tuzo kwa zabuni 32 zenye thamani ya Bilioni 567/- kwa wazabuni wasio na uwezo wa kifedha pamoja na wale waliokosa sifa za kitaalamu za kutekeleza zabuni husika,” amesema Bw. Sando na kuongeza kuwa hatua hiyo imesaidia kuepusha utekelezaji usioridhisha wa miradi unaosababisha upotevu wa fedha za umma na kuchelewesha maendeleo stahiki kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news