Waziri wa Fedha, Dkt.Nchemba awasili Misungwi kwa ziara ya kikazi

MWANZA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) amewasili wilayani Misungwi mkoani Mwanza kwa ziara rasmi ya kikazi na kupokelewa na viongozi na wananchi wa wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo Mhe Dkt. Nchemba atakagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Mwanza na kisha atazungumza na wananchi wa Misungwi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti Katika uwanja wa Amani, Misungwi Mjini.
Mhe. Dkt. Nchemba yuko mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ambayo imelenga kutembelea na kukagua, kuzindua na Kuweka mawe ya msingi katika Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news