Wizara ya Ardhi yaendelea kupunguza changamoto ya usafiri kwa watumishi

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM

CHANGAMOTO ya usafiri inayowakabili watumishi wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi sasa inaenda kupungua kufuatia wizara hiyo kukabidhiwa basi jipya aina ya TATA lenye thamani ya shilingi milioni 170.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Seushi Mbuli akikabidhiwa nyaraka za umiliki wa basi aina ya TATA kutoka kwa Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Limited, Bi. Muareen Kiputa leo tarehe 19 Sept 2024. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Utawala Bw. Simbani Liganga.

Makabidhiano ya gari hiyo yamefanyika jijini Dodoma leo Septemba 19, 2024 baina ya Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Limited, Bi. Muareen Kiputa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi?Seushi Mbuli kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na kuhudhuriwa na baadhi ya watumishi wa wizara Makao Makuu.

Kupatikana kwa basi hilo kuinaifanya Wizara ya Ardhi kuwa na mabasi matatu yatakayopunguza changamoto ya usafiri kwa watumishi wa wizara hiyo hususani pale wanapokwenda na kurudi ofisini sambamba na shughuli nyingine za wizara nje ya makao makuu ya wizara.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Bw. Seushi Mbuli (Wa tatu kulia) na Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Limited, Bi. Muareen Kiputa (wa pili kulia)) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Ardhi Makao makuu mara baada ya makabidhiano ya basi aina ya TATA lenye thamani ya milioni 170.
Muonekano wa basi aina ya TATA lililokabidhiwa kwa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Septemba 19, 2024 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi, Bw. Seushi Mbuli amesema, kupatikana kwa basi hilo kutapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya usafiri kwa watumishi wa wizara hiyo hasa pale wanapokweda na kurudi maofisini.

Ameongeza kuwa, kununuliwa kwa basi hilo ni jitihada za Wizara ya Ardhi kuhakikisha watumishi wake hawapati shida ya usafiri wakati wa kwenda kutekeleza majukumu yao katika maeneo mbalimbali.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi ndani ya basi jipya aina ya TATA (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

‘’Nina imani kubwa sasa changamoto ya usafiri kwa watumishi wetu itapungua sana kutokana na ujio wa basi hili,’’amesema Mbuli.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news