Wizara ya Fedha yaendelea kuwajengea uwezo maafisa ununuzi kuhusu Sheria ya Ununuzi kwa Umma na matumizi ya takwimu sahihi

NA CHEDAIWE MSUYA
WF

WIZARA ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na matumizi Sahihi ya Takwimu kwa Maafisa Ununuzi wa taasisi za umma ili kuhakikisha wana uelewa wa kutosha kuhusu Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Sura namba 410.
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa wakiwa kwenye mafunzo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Mbeya).

Mafunzo haya yanakusudia kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Maafisa Ununuzi wametakiwa kuzingatia sheria hiyo ili kuepuka ukiukwaji wa taratibu na kuhakikisha kwamba miradi yote ya umma inatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia thamani ya pesa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mbeya, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Pascal Manono, alisisitiza umuhimu wa maafisa kuwa na weledi wa Sheria hiyo mpya.
Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma- PPRA, Pascal Manono akizungumza wakati wa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Mafunzo yalihusisha Wakuu wa Vitengo vya Usimamizi na Ununuzi, Ugavi na Wakuu wa Idara za Mipango kutoka Mikoa ya Njombe, Mbeya, Songwe, na Rukwa.
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa wakiwa kwenye mafunzo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

“Sheria ya Ununuzi ya mwaka huu imeweka mkazo maalum kwa makundi maalumu kama watu wenye ulemavu, na kuwapa fursa ya kushiriki katika zabuni za umma kwa kufuata miongozo iliyowekwa.”alisema Bw. Manono.

Katika mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Frola Tenga, alieleza kuwa Sheria hiyo mpya inatoa upendeleo kwa kampuni na wataalamu wa ndani ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki katika miradi ya kimkakati ya Serikali.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Flora Tenga akizungumza wakati wa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

“Lengo ni kuzisaidia kampuni ya ndani kukua na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi kwa kushiriki katika zabuni za umma. Hii itaziwezesha kampuni za ndani kukuza kipato chao na kushindana kikamilifu katika soko la ndani na la kimataifa”. alisema Bi. Tenga

Washiriki wa mafunzo hayo walitoa maoni yao kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kuendelea kusimamia Sheria na kutoa miongozo kwa viongozi wa juu ili kuepuka uvunjifu wa sheria na kanuni zilizowekwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walisema kuwa ni muhimu kwa viongozi wa taasisi za umma kufuata mfumo rasmi wa ununuzi ili kuepuka ukiukwaji wa sheria ambao unaweza kuleta athari kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Bw. Rodrick Mpogole, akizungumza wakati wa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Rodrick Mpogolo, aliwataka Maafisa Mipango kutumia takwimu rasmi na sahihi wakati wa kupanga mipango ya maendeleo.
Alisisitiza kuwa, matumizi sahihi ya takwimu ni muhimu katika kuhakikisha mipango inayowekwa inakidhi mahitaji halisi ya wananchi na kusaidia kukuza uchumi unaoendana na hali halisi ya wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news