NA MAHAMUDU JAMAL
WMA
WAKALA wa Vipimo (WMA) imekabidhi msaada wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala, Septemba 10, 2024 katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

Meneja Muhono amebainisha kuwa, ushirikiano huo baina ya WMA na Jeshi la Polisi umekuwa na tija kutokana na jeshi hilo kudumisha hali ya amani na usalama kwa watumishi wa WMA na wananchi kwa ujumla katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Aidha, ameongeza kuwa, WMA imekabidhi vifaa hivyo ili kuunga mkono matumizi ya TEHAMA kwa taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Polisi na Afisa Mnadhimu wa Mkoa wa Kipolisi Ilala Mohammed Makusi, ameishukuru WMA kwa msaada huo na kusisitiza kuwa Jeshi hilo litaendelea kutumia TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.

Alisema kuwa, Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni Huduma bora za kipolisi zitapatikana kwa kubadili fikra, usimamizi wa sheria na matumizi ya TEHAMA.

