Young Africans Sports Club yaichapa CBE bao 1-0

NA DIRAMAKINI

PRINCE Dube dakika ya 45' ya mtanange kati ya Young Africans Sports Club dhidi ya CBE ya Ethiopia amefanya maajabu.
Ni baada ya kutundika bao pekee ambalo limeiwezesha Yanga SC leo Septemba 14,2024 katika dimba la Abebe Bikila nchini Ethiopia kutwaa alama tatu muhimu katika mechi ya kufuzu kucheza Makundi ya Klabu Bingwa barani Afrika.

Licha ya burudani ambayo mashabiki wa Yanga SC wameipata wakiwa katika dimba hilo, pia bao hilo limewawezesha kuvuna shilingi milioni 5 za goli la hamasa la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news