NA DIRAMAKINI
MWAMBA wa Lusaka, Clatous Chota Chama ndiye aliyefungua ubao wa magoli kati ya Young Africans Sports Club dhidi ya CBE SA ya Ethiopia.
Ni kupitia bao la kipindi cha kwanza dakika ya 35 ndani ya dimba la New Amaan Sports Complex,Zanzibar kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Dakika ya 46, Clement Mzize aliiandikia Young Africans Sports Club bao la pili dhidi ya CBE SA ya Ethiopia.
Aidha, Stephanie Aziz Ki dakika ya 76 74 aliiandikia Young Africans Sports bao la tatu huku upande wa CBE SA wakiwa hawana chochote.
Mudathir Yahya katika dakika ya 87 aligonga msumari wa nne,Duke Abuya dakika ya 90 akagonga mwingine wa tano.
Bao hilo lilidumu muda mfupi ndipo Stephanie Aziz Ki akarejea tena nyavuni kwa kugonga bao la sita, hivyo kuifanya Yanga SC kuibuka kidedea kwa mabao 7-0 dhidi ya CBE SA. Kumbuka bao moja la awali Yanga SC ililipata huko nchini Ethiopia.
Kwa matokeo hayo, Young Africans SC wametinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Pia, kupitia mtanange na CBE SA, Young Africans Sports Club imejikusanyia shilingi milioni 35 kutoka katika bao la hamasa la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.