Zanzibar ina fursa nyingi za uwekezaji-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia wawekezaji kutoka Korea ya Kusini kuwa Zanzibar ina fursa nyingi za uwekezaji na kuwakaribisha kuja nchini.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Septemba 24,2024 Ikulu jijini Zanzibar alipokutana na Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Korea Overseas Infastructure and Urban Development ya Korea Kusini (KiND),Bw.Kim Jong Hoon.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameuambia ujumbe huo kuwa Serikali imefungua milango ya Uwekezaji na Ushrikiano kwa Taasisi zenye nia za kuwekeza nchini na Kuwasisitiza wawekezaji kutoka Korea kuwekeza Zanzibar.Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ameelezea kufarijika kwa taasisi hiyo kuwa na wazo la kuwekeza hapa nchini hususani katika Mradi wa Mchezo wa Maji (Water Park) kuwa wazo zuri na lenye tija.

Rais Dkt. Mwinyi ameuhakikishia Ujumbe huo kuwa Serikali itatoa Ushirikiano wa kutosha kwa taasisi hiyo ili lengo la mradi lifanikiwe.
Naye Bw. Kim Hoon alieambata na Bibi Yoko Eunna ambae ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Usarifu ya Heerim ya Korea amesema Taasisi hiyo ina uzoefu mkubwa wa uwekezaji katika miradi tofauti katika nchi za Afrika ikiwemo Ethiopia na Kenya kwa sasa imevuka kuwekeza Tanzania ikiwemo Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news