Zanzibar itaanzisha mfumo wezeshi kwenye biashara zinazochipukia-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Zanzibar ina kila sababu ya kuanzisha mfumo wezeshi kwenye biashara zinazochipukia zenye uwezo wa kukua kwa haraka ili kustawisha maisha ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua mkutano wa tatu wa pamoja wa taasisi ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera za Kijamii na Uchumi Zanzibar (ZRCP) leo Septemba 17, 2024 kwenye ukumbi wa hoteli ya Madinat Al Bahar Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha, Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa, Zanzibar ina wajasiriamali vijana wenye vipaji wanaochipukia kwenye ujasiriamali, hivyo ni muhimu kuwakuza kwa ajili ya uchumi jumuishi na endelevu wa Taifa.

Halikadhalika, Dkt. Mwinyi amesema,kuna umuhimu mkubwa wa kuwawekea mazingira bora na rafiki wajasiriamali na wafanyabiashara ili wavumbue biashara zenye faida na kuviendeleza vipaji vyao kwa maslahi mapana ya Taifa.
Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa taasisi za Serikali kuzitekeleza kwa vitendo sera na miongozo mbalimbali itakayoanzishwa na ile iliyopo yenye lengo la kusimamia utekelezaji wa maazimio ya kukuza vipaji vya wataalamu kupitia nyanja zote za ubunifu na teknolojia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news