ZANZIBAR-Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF),Hussein Ahmada, amewataka waamuzi watakao chezesha mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu, ikiwemo Ligi Kuu ya Zanzibar (PBZ Premier League) kwenda kusimamia sheria 17 za Michezo wa Mpira wa Miguu ili kuwa na mashindano bora zaidi.
Hussein ameyasema hayo katika kikao na Waamuzi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF).