Ziara ya Rais Dkt.Samia nchini India yaleta matokeo chanya Sekta ya Madini nchini

DAR-Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Madini, Taasisi zake pamoja na Wataalam kutoka Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma wanaotarajia kushiriki mafunzo ya muda mfupi katika Taasisi ya Jiolojia ya nchini India waliagwa rasmi Septemba 2, 2024 katika Ofisi za Ubalozi wa India nchini.
Wataalam hao wanatarajiwa kupata mafunzo ya kujengewa uwezo katika masuala yanayohusu shughuli za utafutaji madini.
Ushiriki wa wataalam katika mafunzo hayo ni matokeo ya ushirikiano kati ya Tanzania na India ambapo yalichagizwa zaidi kufuatia ziara aliyoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Hassan nchini humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news