ZRA yakusanya shilingi bilioni 71 mwezi Agosti

ZANZIBAR-Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) imesema, imefanikiwa kukusanya kiasi ya shilingi bilioni 71.114 mwezi Agosti 2024/2025 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 24.24.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 3,2024 na Kaimu Kamishana Mkuu wa mamlaka hiyo, Said Ali Mohamed wakati akizungumza na vyombo vya habar huko Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Amesema, fedha hizo ni ufanisi wa asilimia 102.34 wa makusanyo yaliyotarajiwa kwa mwezi huo pamoja na kuvuka malengo yaliyowekwa.

Kaimu huyo amesema kuwa, mwezi Agosti 2024/2025 mamlaka hiyo ilikadiriwa kukusanya kiasi ya shilingi bilioni 69.49 ambapo wamefanikiwa kuvuka malengo yaliowekwa na Serikali kwa mwezi huo.

Amesema, makusanyo halisi ya mwezi Agosti mwaka uliopita wa 2023/2024, yalikuwa shilingi bilioni 57.238 ambayo yamekuwa kwa asilimia 24.24 yakilinganishwa na makusanyo halisi ya Agosti,mwaka 2024/2025.

Akielezea sababu zilizopelekea kufanya vizuri amesema, ni pamoja na kuimarika na kuongezeka shughuli za kiuchumi kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, ambazo zinatokana na sera na uongozi mzuri wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan zilizoimarisha mazingira ya biashara kwa pande zote mbili za Muungano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news